MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 17 April 2014

MADARAJA YALIYOBOMOKA KWA MAFURIKO YAANZA KUTUMIKA

Hali ilivyo sasa katika barabara ya Kongowe – Mjimwema – Kigamboni.
Matengenezo yakiendelea katika Daraja la Mpiji.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifuatilia matengenezo katika Daraja la Mpiji.
Hali ilivyokuwa katika daraja la Mto Mtokozi katika barabara ya Kongowe – Mjimwema – Kigamboni.


Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi la Tanzania wamefanikisha kuifungua barabara ya Kongowe kuelekea Mjimwema hadi Kigamboni ambayo ilijifunga kutokana na kukatika kwa kalvati katika mto Mtokozi . Kalvati hilo lilibomolewa na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku kadhaa hapa jijini.

Hapo juzi siku ya Jumanne, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pia alishirikiana na watendaji kwa siku nzima akiwa eneo la Mpiji kuhakikisha barabara ya Dar es Salaam kuelekea Bagamoyo inaanza kupitika tena baada ya kuwa imejifunga kwa takriban siku tatu. Sehemu hii ya barabara iliathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha katika kipindi cha hivi karibuni. Matengenezo katika daraja la Mpiji yalikamilika jana usiku na magari yameanza kupiti bila ya matatizo.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: