WAJUMBE
wa Mkutano Mkuu wa Chadema mkoani Katavi wameridhia kwa kauli moja na kubariki
uamuzi wa kumsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama hicho, John Malack
na viongozi wengine watatu waandamizi wa chama hicho, Jimbo la Mpanda Mjini.

Viongozi hao watatu ni pamoja na
Mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Mpanda Mjini, Seif Sipia, Katibu wa jimbo
hilo, Joseph Mona ambaye pia ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kwa
tiketi ya chama hicho, Said Alfi.
Katika orodha hiyo yupo pia Katibu
Mwenezi wa chama hicho, Godfrey Maufi ambaye ameshavuliwa uanachama wa chama
hicho akidaiwa kuiba nyaraka za siri za chama hicho na kuzisoma katika mkutano
wa hadhara.
Pia mkutano huo umependekeza
kuvuliwa uanachama wa chama hicho watu kadhaa akiwemo Iddi Nziguye ambaye ni
Diwani kwa tiketi ya chama hicho Kata ya Makanyagio na Diwani wa Kata ya
Kashaulili, John Matongo.
Uamuzi huo ulifikiwa juzi na wajumbe
wa mkutano huo mkuu wa chama hicho uliofanyika mjini hapa ukiongozwa na Makamu
Mwenyekiti wa Chadema wa Kanda ya Magharibi, Masanja Mussa Katambi.
Februari 22 mwaka huu kikao cha
mashauriano cha chama hicho ngazi ya mkoa kiliwasimamisha viongozi hao, akiwemo
mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapa, Malack akituhumiwa kufungua na kuhutubia
mkutano wa hadhara uliofanyika Februari 2, mwaka huu ambao unadaiwa
uliwakashifu viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment