MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 23 April 2014

WANANCHI WAPAMBANA NA WASAFARISHAJI WA MAJI TAKA BAADA YA KUYAMWAGA KWENYE MAKAAZI YA WATU


Magari yaliyokuwa yamezuiliwa kwa mawe
Gari ya mizigo ikibeba maji taka kwenye Tanki
 Hatahivyo, wananchi wamelalamikia wahusika kubeba maji taka kwa kutumia SIMTANK, jambo ambalo wamesema ni hatari kwa jamii kutokana na matanki hayo kutokuwa imara na yanaweza kupasuka wakati wowote.
Haya ni maji taka katika eneo lisilostahili
Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao, mwenyekiti wa mtaa wa Ihyolo, Bwana Godwin Tegamaisho amesema kuwa tabia ya umwagaji maji katika sehemu isiyo rasmi limedumu kwa muda wa miezi mitatu hali ambayo ni hatari kwa afya za wananchi.

Afisa tarafa ya Rwamishenye aliyefika kwenye eneo la tukio kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa amesema ni kosa kisheria kumwaga maji taka eneo lisilo rasmi na hao wamiliki wa magari hayo ambayo ni kampuni RWABIZI na mtu binafsi asiyejulikana wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Hatahivyo amewasisitiza wananchi kuwa walinzi wa eneo hilo ili kudhibiti na kuhakikisha yeyote anayekiuka taratibu anakamatwa.

Wahusika waliokutwa na makosa, wamewaomba radhi wananchi kwa kuwalipa fidia ya shilingi laki moja kutokana na muda waliotumia kuzuia magari hayo tangu asubuhi.
Na Mwanaharakati.

No comments: