![]() |
Mbunge Vicky Kamata Hospitali ya
Tabata General, Dar es Salaam jana.
|
Ni matukio nadra kutokea katika
maisha, lakini haya ndiyo yaliyomkuta Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky
Kamata, baada ya kuugua ghafla saa 36 kabla ya harusi yake.
Kuugua kwa bibi harusi huyo
mtarajiwa, kumezua gumzo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na maeneo
mengine nchini, kutokana na kile kilichoelezwa kwamba harusi hiyo ilipangwa
kuwa ya kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni
Kamata ilikuwa afunge ndoa jana
katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza Dar es
Salaam na tayari kadi za mialiko zilishasambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo
wabunge.
Habari za kuugua ghafla kwa mbunge huyo ambaye pia ni msanii
wa muziki aliyetamba na kibao chake cha ‘Wanawake na Maendeleo’ zilianza
kuzagaa kwa kasi juzi jioni nchini.
Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake, aliugua usiku wa kuamkia jana na kupelekwa katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea ambapo amelazwa.
Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake, aliugua usiku wa kuamkia jana na kupelekwa katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea ambapo amelazwa.
“Niliugua tumbo ghafla, nilipata
maumivu makali sana nikampigia daktari wangu na nilipomweleza jinsi
ninavyojisikia, aliniambia niende hospitali haraka na kutokana na hali ilivyo,
waliamua nilazwe,” alisema Kamata akiwa kitandani katika hospitali hiyo.
Kamata alifafanua kuwa, pamoja na
mambo mengine, hali yake ya ujauzito imekuwa ikimsumbua na kuchangia yeye
kulazwa kwa mara ya pili sasa katika kipindi cha wiki mbili. Mbunge huyo ambaye
alitakiwa kufunga ndoa leo, alisema kuwa kutokana na maradhi hayo, haelewi
hatima ya ndoa yake, ingawa wanafamilia na wanakamati wanaendelea na mipango ya
harusi kama ilivyopangwa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment