MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday 21 May 2014

MASWALI NANE KUHUSU KUZAMA MV BUKOBA

 Tarehe na mwezi kama wa leo ikiwa ni (21. May. 1996) ajali, ajari kubwa ya majini ilitokea alfajili hiyo maili chache kutoka bandari ya mwanza mjini.

Meli kubwa ya mv bukoba iliyoundwa mwaka 1979 na iliyokuwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430ilizama maji na zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha baada ya KUTOBOLEWA kwa meli hiyo ambayo tangu kuundwa kwake hadi kuzama kwake ilikuwa na umri wa miaka 17 tu.

Leo tarehe 21. 05. 2014 watanzania "tunakumbuka" miaka mingine 17 tangu kuzama kwa meli hiyo. Tarehe kama ya leo mwaka 1996 mji wa mwanza uligubikwa na simanzi ya kutisha.



1: Je, tulijifunza jambo lolote kutokana na ajali hiyo?

2: Yanayotokea yanafanyiwa kazi?

3: Je kuna hali yoyote ya uwajibikaji (kwa waliopewa dhana ya kusimamia sheria) katika kuzingatia sheria za usafiri na usafirishaji wa majini na nchi kavu leo?

4: Je, tumekwishajijengea hali ya kuchukua hatua za uokoaji pale tunapopatwa na majanga ya majini au nchi kavu leo??

5: Je, taarifa/ripoti ya uchunguzi wa ajali hiyo ilifanyiwa kazi ipasavyo??

6: je, ni ajali ngapi za vyombo vya majini zimetokea tangu kuzama kwa meli hiyo?

7; Kama kuna funzo lolote mbona ajali zinaendelea kutokea ndani ziwa Victoria?
8: Naodha aliyekuwa akiongoza meli hiyo ni nani na taarifa zake ziko je?
 

Na Mwanaharakati.

No comments: