
Akizungumza
mara baada ya kutembelea bandari hiyo pamoja na eneo linalohifadhia makontena
matupu karibu na hoteli ya Bwawani wilaya ya mjini Unguja, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alisema kwa ujumla hali
hairidhishi katika bandari hiyo kutokana na msongomano wa makontena.
“Bandari
haina nafasi ya kuweka makontena yote yanayoingia na yanayotoka. Hali
hainiridhishi mimi na kila mtu hapa. Kwa mfano leo hii bandarini kuna meli
inashusha makontena karibu 350 mengine yakijazana kila mahala mpaka hapa
Bwawani” Dk. Shein alifafanua.
Alijibu
swali kuhusu madhumuni ya ziara hiyo alisema ilikuwa ni kuona maeneo yote ya
bandari yakiwemo ya kuwekea makontena na pamoja na maghala mbalimbali ili kuona
kipi kinaweza kufanyika kupata eneo kwa ajili ya kuondoa tatizo la msongomano
wa makontena katika bandari hiyo.
Aliukumbusha
uongozi wa Shirika hilo kuwa sehemu ya kuwekea makontena la Bwawani ni ya muda
tu kama ilivyokubaliwa wakati wa uongozi uliopita wa Shirika hilo
ulipokabidhiwa eneo hilo hivyo ana hakikika kuwa tangu wakati huo walikuwa
wanafanya mipango mbadala wa kupata eneo jingine.
Alifafanua
kuwa eneo hilo limo katika mpango wa Serikali wa uwekezaji kwa shughuli
nyingine za maendeleo ambapo wakati wo wote linaweza kuchukuliwa kwa shughuli
hizo hivyo uongozi wa bandari hauna budi kuzingatia hilo kwa kuharakisha mipango
yake ya kuondoka katika eneo hilo.
Hata hivyo
Dk. Shein alikiri kuwa Bandari ya Malindi hivi sasa imeshakuwa ndogo na itakuwa
vigumu kukidhi mahitaji ya matumizi ya sasa ya bandari hasa baada ya mfumo wa
usafirishaji wa bidhaa kubadilika kuwa wa kutumia makontena.
Kwa hiyo
alieleza kuwa ndio maana jitihada za Serikali zimeelekezwa katika kutekeleza
mpango wake wa ujenzi wa bandari mpya na ya kisasa huko katika eneo la
Mpigaduru liliko kilomita chache kutoka bandari ya sasa ya Malindi.
Katika ziara
hiyo Dk. Shein amelitaka Shirika hilo kuangalia upya matumizi bora ya baadhi ya
majengo yake kwa kuyajenga upya ili kupata ofisi za kisasa na bora ili Shirika
liweze kutoa huduma vizuri kwa wateja wake.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Bwana Abdalla Juma Abdalla alisema
lengo la kuhifadhi makontena matupu katika eneo la Bwawani ni kutoa nafasi kwa
makontena yenye bidhaa kuweza kushushwa kutoka melini na kuokoa gharama na
usumbufu pindi makontena hayo yakichelewa kushushwa kutoka melini.
Alibainisha
kuwa Shirika lake inalipa kipaumbele suala la kuondosha msongomano wa makontena
bandarini hapo na kwamba uongozi wa bandari wakati wote umekuwa ukihakikisha kunakuwepo
na ufanisi katika utendaji wake.
Katika ziara
hiyo Dk. Shein alifuatana na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Miundombinu
na Mawasiliano, Wizara ya Kilimo na Maliasili pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment