
Inahofiwa kuwa kuna maiti zaidi zilizonaswa kwenye vifusi vya majengo yaliyo poromoka kutokana na shambulio hilo.
Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo lakini wengi wanaamini kuwa Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram lilihusika.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amejitokeza kukemea mashambulio hayo na kusema kuwa amejitolea kuangamiza kabisa ugaidi.
Mji wa Jos unatazamiwa kuwa mji mkuu wa jimbo la
Plateau ambalo liko katika eneo la katikati linalo tenganisha kaskazini iliyo
na raia wengi zaidi wa kiislamu, na kusini lililojaa wakristu zaidi.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment