
Mkataba huo
ulisainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya
Serikali ya Tanzania na Balozi wa EU nchini Filberto Sebregond leo jijini Dar
es salaam.
Akizungumza
baada ya kutia saini mkataba huo, Dkt. Likwelile alisema kuwa sehemu ya msaada
huo ambao ni Shilingi Bilioni 82.4 ambazo ni sawa na Euro milioni 36.5 utatumika
kuendeleza sekta ya kilimo na kukuza uchumi nchini kwa kupitia kituo maalum cha uendelezaji kilimo ukanda wa
Kusini Tanzania (SAGCOT) na kuboresha miundombinu ya barabara za ukanda huo.
Vilevile Dkt.
Likwelile alisema kuwa sehemu iliyobaki ya msaada huo ambao ni Shilingi Bilioni
51.9 ambazo ni sawa na Euro milioni 23 itatumika kuimarisha biashara na
ushirikiano katika jumuiya kwa kuanzisha
kituo cha pamoja cha ukaguzi mipakani (OSIS).
“Vituo hivyo vya
ukaguzi mipakani vitakuwa na manufaa si kwa Tanzania tu, bali hata katika nchi
mbalimbali zinazopakana na Tanzania” alisema Dkt. Lkwelile.
Alifafanua kuwa msaada
uliosainiwa unamanufaa kwa wananchi kwa kuboresha miundombinu vijijini na kusambaza
umeme vitu ambavyo vitasaidia kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Naye Balozi wa EU
nchini Filberto Sebregond alisema kuwa anaamini msaada huo utasaidia juhudi za
Serikali ya Tanzania katika kuongeza nafasi za ajira, kupungua kwa bei za
bidhaa mbalimbali na kuendelea kukuza uchumi nchini.
Balozi huyo
alisema kuwa EU inaamini kuwa ushirikiano wake na Tanzania utaendelea kuimarika
kwa kuhimiza maendeleo kwa pande zote mbili na amani ya watu wake.
Hafla hiyo ya
kusaini mkataba ilihudhuriwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Fedha, Nishati na
Madini, Uchukuzi na Ujenzi, EAC, DFID, SAGCOT, wajumbe kutoka EU, Shirika la
maendeleo ya Ufundi kutoka Ubelgiji na washirika wa maendeleo.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment