NEWS ALERT!!!MGOGORO BUKOBA; WAZIRI MKUU ASISITIZA ANATORY AMANI SIYO MEYA TENA
Ameongeza kuwa baada CAG kubaini mapungufu makubwa yaliyojitokeza katika utekelezaji wa miradi na kusaini mikataba, ofisi ya waziri mkuu kupitia naibu waziri wa TAMISEMI Agrey Mwanri, ilimtaka Meya huyo kujiuzulu kwa kujipima mwenyewe na alifanya hivyo ambapo ofisi ya waziri mkuu iliandika barua kuthibitisha hivyo na kupitia vyombo vya habari, hivyo anashangaa kusikia mpaka zinafunguliwa kesi kukwamisha maendeleo ya wananchi.
 |
| Bwana Anatory Aman |
Bwana Amani alisema kuwa amesikia maelekezo ya serikali hiyo ameyatii na kuchukua hatua iliyopendekezwa, lakini baadaye akaitisha Press conference akiwa Mwanza na kusema kuwa yeye hakutangaza kujiuzulu na atakuwa nje ya ofisi kwa siku kadhaa hivyo kumsihi aliyekuwa naibu Meya aendelee kushika nafasi hiyo.
Madiwani wengine walipojipanga kuendelea na vikao ili kuendeleza kazi ya wananchi, diwani wa Kahororo Chief Karumuna, alifungua kesi mahakamani ambayo mpaka sasa inaendelea hivyo kusimamisha vikao vyote vya madiwani.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment