
Kwa mujibu wa taarifa bomu la mkono
lilitupwa kwenye basi katika kituo cha mabasi cha Mwembe Tayari ambao hupendwa kutembelewa
na watalii na kusababisha vifo hivyo na wengine kujeruhiwa.
Mlipuko mwingine umetokea katika
mtaa wa kifahari wa Nyali.
Kamishna mkuu wa polisi Mombasa,
Nelson Marwa, amesema watu 6 wamejeruhiwa na kuwa watu waliotekeleza shambulizi
hilo walitoroka kwa Pikipiki.
Kenya imekuwa ikikumbwa na matukio
ya mashambulio yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la kiislamu la Alshabaab la
nchini Somalia.
Aidha nchi hiyo imekuwa katika
tahadhari tangu mwezi Septemba mwaka jana ambapo wanamgambo wa Alshabaab walivamia
kituo cha biashara cha Westgate kilichopo mji mkuu wa Nairobi na kuua watu
wapatao 67.
Al Shabaab ni kundi ambalo lina
uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda ambalo limeapa kulipiza kisasi
kufuatia Kenya kutuma majeshi yake nchini Somalia mwaka 2011ambayo yameungana
na yale ya Umoja wa Afrika AMISOM.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment