
Akitoa taarifa hii kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime amesema kuwa mnamo tarehe 18/5/04 majira ya saa kumi jioni katika kitongoji cha mkwawa Kata ya mpunguzi Jofrey Mkalabure ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi.
Mpunguzi alikanyagwa na tembo waliovamia kitongoji hicho na kumsababishia mauti.
Aidha
Kamanda Misime amesema Tembo hao walimvamia Bi. Elizabet Mgawa mwenye
umri wa miaka 89 na kumsababishia majeraha mbalimbali katika sehemu zake
za mwili na punde baada ya kupelekwa hospital ya mkoa wa Dodoma kwa
ajili ya matibabu alifariki.
Kamanda
Misime ameongeza kuwa katika tukio hilo jumla ya watu watano wamejeruhiwa
ambapo wote wametibiwa na kuruhusiwa.
Kamanda
wa polisi ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi
pamoja na idara ya wanyama pori kwa kutoa taarifa pindi watakapowaona tembo hao
na kutokuwafuata tembo hao wala kuwapigia kelele.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment