TAARIFA KWA UMM;-TAARIFA YA
BAADHI YA WAJUMBE WA BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU CHADEMA MIKOA YA DSM, PWANI NA
TANGA KUPINGA UHUNI WA KISIASA UNAOITWA UKAWA. UTANGULIZI.
Ndugu
wanaHabari, Tunapenda mtusaidie kufikisha ujumbe wetu huu kwa umma unaotokana
na malalamiko na manung’uniko ya
wanachama wenzetu wa CHADEMA
kuhusu udhaifu
mkubwa wa kiuongozi unaoendelea kwa sasa chini ya mwavuli wa UKAWA.
Kwa wiki
kadhaa sasa, kumeibuka msamiati mpya wa kisiasa wa UKAWA uliopelekea mpaka
kuundwa kwa BARAZA KIVULI LA UKAWA pale Bungeni bila kufuata Utaratibu. Sisi
viongozi ambao miongoni mwetu ni Wajumbe wa vikao halali vya chama, ambavyo ni
Baraza Kuu na Mkutano mkuu wa chama kutoka mikoa ya Tanga, Pwani na DSM kwa
masikitiko makubwa tunasema kuwa hatupendezeshwi na mwenendo huu wa chama
unaofanywa na viongozi wetu wakuu.
KUSUSIA BUNGE LA KATIBA.
Ndugu
wanaHabari, Kwa namna ambavyo tumepambana kwa miaka mingi kudai na kuishinikiza
serikali kuridhia uandikaji wa katiba mpya, ni mpumbavu pekee anayeweza kususia
fursa ya uandishi huo tena kupitia chombo huru (BUNGE LA KATIBA) kwa sababu tu
ya mgongano wa kimaslahi. Tunasikitika sana kuwaona viongozi wetu na wabunge wa
chama chetu cha CHADEMA wamesahau kazi tuliyowatuma ya kwenda kuandika katiba
mpya yenye kuzingatia maslahi ya wananchi badala yake wamekwenda kupigania
vyeo.
Tumefedheheshwa
sana na namna ambavyo wawakilishi hawa wamekubali kutanguliza mbele maslahi yao
na kuyaacha maslahi ya wananchi ambao ndio waliuowatuma, kwenye Rasimu yenye
sura zaidi ya 18 ni uzezeta kususia sura 2 tu za mwanzo kisa tu maslahi yao ya
kugawana vyeo wanaona hayawezi kutekelezeka.
Tunaomba
ifahamike kwamba, hakujawahi kukaliwa kikao chochote halali cha chama chetu
kilichoazimia na kuwaagiza wajumbe wanaotokana na chama chetu wasimamie katiba
yenye SERIKALI TATU, na ikionekana haiwezekaniki WASUSE NA KUTOKA NJE YA BUNGE.
Huu ni udhaifu unaotawaliwa na uroho wa madaraka, sisi kama viongozi halali wa
kikatiba wa chama hatujawahi kuwaza wala kuamua kuhusu ujinga huu, siku zote
tumekuwa tukiwasisitiza wajumbe wetu kwenye fursa yoyote watakayoipata kwenda
kusimamia mawazo na misimamo ya wananchi ambao ni wanyonge,
Tunawatuma
wajumbe wetu kuhakikisha tunapata katiba itakayosimamia na kuzitunza Rasilimali
zetu, na wala si kweli kuwa Idadi ya Serikali kama ni 3 au 2 au 5 au zozote
inaweza kuwa muarobaini wa changamoto zetu. Daima dumu tumekuwa tukiamini
kwenye mapambano ya Hoja ambayo ndio msingi mkuu wa demokrasia ya kweli
Tunayoisimamia kama CHADEMA.
Hivyo Basi
tunasema, si sahihi hata kidogo kwa wajumbe wetu wa Bunge la katiba kususia
vikao vile na ndio maana hata baadi ya wabunge wengi wa chama chetu wamekuwa
wakilalamika chini chini kwetu sisi wajumbe wa baraza kuu kwamba wamechoka sasa
kuburuzwa na viongozi wakuu wa chama na kwamba wao nao wana mawazo na misimamo
yao, sasa kwa niaba yao pia tumeona kama viongozi wa chama tulikemehe hili.
Nipo tayari
kuyataja majina ya wabunge hawa wanaolalamika kuburuzwa ambao ni zaidi ya
wabunge 31 wa kuchaguliwa na wa viti maalum. Muungano wetu huu wa UKAWA ni
muungano wa kinafiki usiokuwa hata na hadidu za rejea, hakunaga muungano
duniani kote ambao waunganaji wake wanaungana kiujanja ujanja tu kama
walivyofanya viongozi wetu hawa. Hatuungi mkono na tunawataka wasiendelee na
upuuzi wao huu, warudi bungeni kama hawataki wajitoe tuchague wabunge wengine
watakaowawakilisha wananchi wanaotuamini. Ni sawa na ndoa ya mkeka, hakuna
maridhiano, hakuna vikao, asubuhi wapenzi jioni wana ndoa, ndoa ya namna hii
kamwe haiwezi ikadumu hata kidogo.
BARAZA KIVULI LA UKAWA.
Tunasikitika
sana na kitendo cha mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe, kutufanya sisi
wajumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu hatuna maana kwenye kufanya maamuzi ya
chama. Walituaminisha kwamba CUF wamefunga ndoa na CCM na kwamba wao ni sehemu
ya serikali hivyo hawawezi kushirikiana na chama ambacho ni sehemu ya serikali,
kwa msingi huu tukaazimia kwenye vikao vya chama ambavyo ni halali kwamba chama
chetu hakitashirikiana na chama kingine chochote cha siasa kwa kuwa ni
washirika wa CCM na kwamba wao ni CCM-B Tumemkashigu na kumtuhumu James Mbatia
na NCCR nzima kuwa ni Tawi la CCM na ndio maana hata Mbatia ameteuliwa kuwa
Mbunge, inakuwaje leo tunashirikiana na watu hawa ambao wanatumiwa na CCM?.
Ni lini
Muungano wa CCM na CUF umevunjika rasmi?. Ni lini ushirikiano wa NCCR ya MBATIA
na CCM umekufa rasmi?. Je mazingira yaliyofanya tuwahesabu wenzetu hawa kuwa ni
CCM B leo yamebadilika?, na kama yamebadirika yamebadilika lini na
yamebadilikaje?.
Je sio kweli
kwamba tuliwatenga wenzetu na kuwakashifu kwa sababu tu ya uchu wa madaraka?.
Yaani sio kweli kwamba tuliwafedhehesha wenzetu hawa kwa sababu ya UWAZIRI
KIVULI?. Na leo tunawasafisha wenzetu hawa kwa UWAZIRI KIVULI HUO HUO.
Kwanini
viongozi wetu wanakuwa na UCHU na UROHO wa MADARAKA kiasi hiki?. Kama tunaweza
tukawaita wenzetu MASHETANI asubuhi na jioni tukawaita MALAIKA kwa sababu ya
UWAZIRI KIVULI, je tukipewa nchi na kushika dola, si Tutawaita wenzetu majina
mabaya zaidi?. Si tutakuwa na serikali mbovu nay a ajabu zaidi ya hivi sasa
tulivyo kwenye siasa za upinzani tu tulio nao?.
Kwa misingi
huu, Tunaamini kuwa UKAWA ni UNAFIKI WA KISIASA, na umebuniwa kwa sababu moja
tu nayo ni kugawana vyeo, hakuna sababu yoyote yenye mantiki iliyopo kwenye
uundwaji wa UMOJA huu na ndio maana hauna hadidu za rejea wala hauna hati za
makubaliano miongoni mwetu. Napenda kuwaambia watanzania kuwa sisi baadhi yab
wajumbe wa Baraza kuu na mkutano mkuu wa mikoa ya Pwani, Dsm na Tanga hatuungi
mkono upuuzi wowote wenye lengo la kusimamia ugawanaji wa vyeo na madaraka,
watu wa namna hii tunawaita WALAFI wa MADARAKA.
Tunaunga mkono
watanzania wote wanaoitakia heri Tanzania yetu. Mungu ibariki Tanzania
Imeandaliwa na Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Mikao ya
Pwani, DSM na TANGA Na imesomwa nami
……………………………………………………
JOSEPH YONA PATRICK +255713802226
Mwenyekiti wa CHADEMA WILAYA YA
TEMEKE Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa TEMEKE MJUMBE WA BARAZA KUU CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA KAMATI YA UTENZAJI
BAVICHA TAIFA
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment