MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 20 May 2014

MAZISHI YA MSANII ADAM PHILP KUAMBIANA


 

Nyota wa filamu aliyefariki dunia ghafla  Jijini Dar es Salaam, Adam Philip Kuambinana, anatarajiwa kuzikwa leo Jumanne kwenye makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Kwa Mujibu wa mratibu wa shughuli hiyo ya mazishi Steve Nyerere, Mwili wa Marehemu Adam Philip Kuambiana utapelekwa viwanja vya Leaders leo Jumanne kwa ajili ya wadau ndugu jamaa na marafiki kuuaga kabla ya maziko.

Marehemu Kuambiana alifarki dunia akiwa njiani kuelekea hospitali ya Mama Ngoma Mwenge Dar es Salaam baada ya kuanguka akiwa kwenye upigaji picha filamu katika hoteli moja iliyopo eneo la Sinza. 

Inadaiwa kabla ya umauti kumfika marehemu alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Adam Kuambiana mahali pema peponi Amina.

Na Mwanaharakati.

No comments: