Msanii wa filamu nchini, Dr Cheni
amelazwa toka jana katika hospitali ya Buruhani jijini Dar es Salaam kutokana
na ugonjwa wa Dengue.
Akizungumza na waliomtembelea,
amesema kuwa bado hali yake sio nzuri kutokana na kuishiwa damu na mwili
kupoteza nguvu.
“Bado ni
nipo hospitali ya Buruhani naumwa hili gonjwa jipya,sijui unaitwa Dengue,” amesema. “Bado hali
yangu sio nzuri kabisa,yaani naumwa, napungukiwa damu, mwili unauma, kwahiyo bado
ninaumwa, hii homa ilinianzia wiki iliyopita sema ilikuwa bado hawajaigundua
ila jana ndio wameingundua,” ameongeza.
Dr Cheni amesema kuwa anawaomba
Watanzania wamuombee kwani bado hali yake sio nzuri.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment