Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA). 

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue, uteulzi huu umaanza tarehe
06 Mei, 2014. Bwana BADE anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu tarehe 14
Desemba,2013.
Kabla ya uteuzi
huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangu
Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania tangia Bwana Kitilya alipostaafu.
Kabla ya
kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya kazi
katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya fedha
na mapato kama ifuatavyo:-
Ø
Oktoba, 1995 –
Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.
Ø
Juni, 2000 –
Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.
Ø
Juni, 2001 –
Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.
Ø
Septemba, 2001 –
Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).
Ø
Januari, 2007 –
Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)
Ø
Desemba, 2009 –
2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays Bank
Plc Emerging Markets.
Ø
Novemba, 2010 –
Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance Company.
Bwana Rished
BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and Management ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of Commerce in Banking and Finance
ya Chuo Kikuu cha Sydney (1999), na ni Certified Public Accountant (CPA).
Katika kumteua
kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa Rais ana imani
kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa kushirikiana
na watumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwa kuzidi kuimarisha
Mamlaka hiyo na kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya Serikali
kwa faida ya Taifa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment