Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt Laurent M. Shirima kuwa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA).
Dkt. Shirima ni Mkurugenzi wa kujenga
Uwezo wa Huduma za Ushauri (Capacity Building and Advisory Service-PPRA) na pia
ndiye anaye kaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa PPRA.
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue, Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2014.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment