![]() |
| Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na ujumbe wa watu kutoka Congo hawapo pichani waliomtembelea ofisini kwake kuwaalika wasanii kutoka Tanzania |
![]() |
| Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akifafanua jambo kwa wajumbe wa maandalizi ya fiesta kutoka Congo walipomtembelea ofisini kwake |
Wasanii wa muziki
nchini waalikwa kushiriki katika sherehe za fiesta nchini Congo zinazotarajiwa
kufanyika julai 16 hadi 26 mwaka huu.
Mwaliko huo umetolea na
wajumbe kutoka Congo walioshiriki katika siku ya Uanuwai wa Utamaduni duniani
iliyoadhimishwa kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam
na baadaye kumtembelea Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt
Fenella Mukangala ofisini kwake ambapo
walimuomba wasanii wa muziki kutoka Tanzania kushiriki sherehe fiesta
zitakazofanyika nchini Congo mwaka huu.
Akitoa ufafanuzi
kuhusiana na sherehe hizo Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne
Gizenga amesema kuwa lengo la sherehe za fiesta mwaka huu ni kuwakutanisha
wasanii wa Afrika wanaoishi nchi za maziwa makuu ili waweza kupata nafasi ya
kupanda mti wa amani ikiwa na lengo la kuziwezesha nchi hizo kuwa na mazungumzo
ya amani.
Bi. Gizenga amesema
kuwa wanatarajia kupata wasanii wa muziki kutoka nchini Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda, Burundi pamoja na wasanii wa Congo watakaoshiriki fiesta ndani
ya mikoa miwili nchini Congo katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini Goma pamoja na
Kivu ya Kusini Bukavu.
“Tumezunguka nchi
zilizopo katika maziwa makuu tukiwaomba wasanii wa nchi hizo kushiriki katika
sherehe za fiesta nchini Congo ambazo mwaka huu tutahusisha upandaji wa mti wa
amani tukizitaka nchi hizo ziwe na mazungumzo ya amani na mshikamano” alisema
Bi. Gizenga.
Kwa upande wake waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
amewashukuru wajumbe hao kwa mwaliko na kuwahaidi kuwa wasanii kutoka nchini
Tanzania watapata fursa ya kipekee hivo ni muhimu kwao kushiriki ili waweze
kuiwakilisha Tanzania na kuweza kupata uzoefu kutoka nchi jirani.
Aidha Dkt. Mukangara
amesema kuwa ni muhimu kwa Tanzania kushiriki katika sherehe hizo kwani
Tanzania ilishiriki kwa kiasi kikubwa katika kuleta amani ya nchi ya Congo
hivyo aina budi kushiriki na kuendeleza amani na mshikamano wa nchi hizo mbili.
Na Mwanaharakati.



No comments:
Post a Comment