Ni baada ya kuahidi kujenga kituo katika kata Muhutwe mwaka jana na hawajafanya hivyo.![]() |
RPC KAGERA- MAYUNGA |
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera GEORGE
MAYUNGA ameagiza waganga wote wilayani muleba wasakwe na kukaguliwa vibali
vyao.
Kamanda MAYUNGA
amesema hayo Siku moja baada ya mganga wa kienyeji kukamatwa na jeshi la
polisi na kukiri kuhusika na tukio la mauaji ya mtoto wa miaka nane.
![]() |
MGANGA ANAYTUHUMIWA |
Kamada MAYUNGA amemuagiza mkuu wa kituo cha polisi
muleba kuhakikisha ndani ya muda mfupi ambao hakuutaja kuhakikisha wanabainisha ni waganga wangapi
waliopo wilaya ya Muleba na niwangapi wanapiga lamuli za uchonganishi kama
alivyokuwa anafanya mganga huyo aliyekamatwa.
Ameongeza kuwa waganga wanaopiga lamuri ni
wachonganishi ndio wanaochochea vurugu
katika jamii ikiwa ni pamoja na kusababisha mauaji ya watu wakiwemo maalubino,
vikongwe na watoto.
![]() |
ALIYEKUWA RPC KAGERA- KALANGI |
Aliyekuwa kamanda wa polisi mkoani Kagera wakati huo Philp Kalangi pichani, aliahidi kuweka kituo cha polisi katika eneo hilo, kutokana na wananchi kuwa walikuwa wameshaamua kuwa wanajifungia mapema kabla ya saa moja kutokana na vifo hivyo vya kutekwa kuchinjwa na kuchunwa ngozi.
Hivyo wakati kandayaziwa blog ikiendelea kufuatilia, itajikita zaidi kujua kwanini ahadi ya polisi haitekelezwi ilhali vifo vikiendelea.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment