
Akizungumza Ikulu mjini Lilongwe
muda mfupi uliopita ameiamuru Tume ya uchanguzi MEC kusitisha shughuli hiyo na
kutangaza kuwa uchaguzi urudiwe ndani ya siku 90 kutoka leo na kwamba yeye
hatogombea tena urais wa nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza
amearifu kutoka mjini Lilongwe kuwa Dr Banda amesema amelazimika kuchukua hatua
hiyo kutokana na kile alichokiita kuvurugwa kwa mtiririko mzima wa shughuli za
upigaji kura,kuhesabu na hata namna ya kusimamia utoaji wa matokeo yake.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya
Malawi Jaji Mackson Mbendera amesema kuwa anawasiliana na mwanasheria mkuu wa
serikali ili kuangalia uwezekano wa amri hiyo ya Rais kutekelezwa na kama
haijavunja sheria ya nchi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment