
![]() |
|
Msururu wa magari ukiwa mkubwa katika eneo hilo na wasafiri mbalimbali wakitoka kuangalia tukio
hilo baada ya kushindwa kupita kutokana na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka.
|
Lililipuka majira ya Saa 11:00 katika barabara kuu
ya Dodoma Mwanza eneo la Shelui mkoani Singida, wakati breki za tanki hilo
upande wa kushoto zilipojam na kusababisha moto, na kumsababishia dereva wa lori
lenye namba za usajiri T 164 CGF aina ya Scania lililokuwa likivuta tanki hilo
kusimamishwa na kukata haraka tanki hilo huku akiondoa haraka injini ili
kuepusha madhara zaidi ambayo yangeweza kutokea.
Tukio hilo lilisababisha usumbufu mkubwa kwa abiria
na msururu wa magari kushindwa kupita katika eneo hilo, kutokana na moto mkubwa
uliochanganyika na moshi kutishia usalama wa watumiaji wengine, hata hivyo
baada ya moto kupungua askari wa usalama barabarani waliamuru magari yaanze
kupitia pembeni mwa barabara hiyo ili kuendelea na safari hakuna mtu
aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo.
Na Mwanaharakati.


No comments:
Post a Comment