Kamishna
kova ameamua kuitoa hadharani picha ya mtuhumiwa huyo mbele ya wanahabari ili
apatikane mara moja
Jeshi la Polisi Kanda Maalum
D’Salaam limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa mhimu ambaye ni kinara wa mtandao wa
wizi katika mabenki ambaye anajulikana kwa jina la RONALD S/O MOLLEL umri miaka
37, mfanyabishara na mkazi wa Kimara Bonyokwa Jijini D’salaam.
Mtuhumiwa huyu amekimbilia mafichoni
mara baada ya tukio la ujambazi katika Tawi la Benki ya Barclays
Kinondoni lililotokea tarehe 15/4/2014 ambapo majambazi walifanikiwa kupora
kiasi kikubwa cha fedha T.Shs.390,220,000/= , USD 55,000/= na EURO
2150/=.
Aidha sasa imefahamika kwamba
mtuhumiwa huyu ni mume wa mtuhumiwa wa kwanza katika tukio la Barclays Benki
aitwaye ALUNE D/O KASILILIKA @ ALUNE D/O MOLLEL , miaka 28, Mkazi wa
Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa Benki Tawi la Barclays Kinondoni.
Mtuhumiwa Mollel anatafutwa kwa kila
hali kwa vile yeye ndiye alikuwa kinara wa kupanga tukio hilo la Barclays na
mara baada ya tukio ametoroka na kiasi kikubwa cha fedha hizo zilizoibiwa.
Jeshi la Polisi limelazimika kutoa
picha yake hadharani kwa kutumia dhana ya ulinzi shirikishi ili mtuhumiwa huyu
akionekana akamatwe na taarifa zitolewe katika kituo chochote cha Polisi ikiwa
ni lengo la polisi kupambana na uhalifu katika dhamira ya kuzuia uhalifu,
kulinda maisha na mali za wananchi.
Zawadi nono ya fedha taslim
itatolewa kwa siri kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa
kwa mtuhumiwa huyu. Pamoja na maelezo hayo mtuhumiwa mwenyewe sasa
anapewa fulsa ya kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kabla ya
kukamatwa kwa njia nyingine.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment