
Mpango wa matokeo makubwa sasa
katika Sekta ya Elimu nchini,uongozi wa shule ya msingi majengo wilayani Kahama
mkoani Shinyanga umeanzisha mbinu mpya ya ufanyaji mitihani kwa wanafunzi wao
mbinu ambayo imepokelewa kwa mtazamo tofauti na baadhi ya wazazi wenye watoto
katika shule hiyo.
Licha ya kuwa shule hiyo ina
madawati ya kutosha uongozi wa shule hiyo umeanzisha mbinu hiyo mpya ambapo
wanafunzi wanafanya mitihani yao wakiwa wamekaa chini katika uwanjani wa shule
hiyo bila madawati huku wakiwa umbali wa mita mbili kila mmoja na
kuandikia kwenye magoti na chini ya mchanga.
Wanahabari
wamekuta wanafunzi wa darasa la tatu na la
nne wakifanya mtihani wa kufunga muhula wa kwanza chini ya vivuli vya miti
katikati ya uwanja wa shule hiyo majira ya saa mbili asubuhi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo William
Ngulu alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi wa sababu ya wanafunzi kufanya
mitihani chini licha ya kuwa shule hiyo ina madawati ya kutosha alisema kuwa
hiyo ni mbinu ya kuwafanya wanafunzi wake wafanye mitihani kwa akili binafsi
bila kuangaliziana.
Ngulu ameongeza kuwa mitihani hiyo
hufanyika mida ya asubuhi tu wakati jua likiwa halijawa kali na kwamba hali
hiyo inaleta mafanikio makubwa katika shule yake katika kufikia mpango wa
matokeo makubwa sasa (BRN) BIG RESULT NOW.
Katika hatua nyingine Mwl Ngulu
amesema kuwa mbinu hiyo wameanza kuitumia toka mwaka 2013 na ndiyo siri ya
mafanikio ya shule hiyo kuwa ya kwanza kiwilaya katika matokeo ya darasa la
saba mwaka 2013.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa majengo
ambaye ni mzazi katika shule hiyo Noel Mseveni amesema kuwa
swala hilo si jema na kwamba Kitendo hicho ni kuwazalilisha watoto na wazazi na
kutoa mbinu mbadala ambapo ameshauri wanafunzi hao wafanye mitihani kwa awamu
mbili za asubuhi na jioni ili kuwapa fursa wote wafanye mitihani wakiwa
wameketi kwenye madawati.
Kwa upande wake Afisa elimu msingi
katika halmashauri ya mji wa Kahama Aluko Lukolela Aluko amesema
kuwa mbinu hiyo ameianzisaha yeye alipohamia wilayani hapo na kwamba imeleta
mafanikio makubwa katika kuinua elimu.
Sambamba na hayo Aluko amepinga
mbinu mbadala iliyotolewa na Mwenyekiti wa mtaa huo na kusema kuwa mbinu hiyo
itasababisha kuvujisha mitihani hiyo kwani wanafunzi watakaofanya asubuhi
watakuwa na nafasi kubwa ya kuwaambia maswali wenzao watakaoingia jioni.
Mbinu hiyo mpya iliyoanzishwa mjini
kahama katika kuhakikisha wanafunzi wanafanya mitihani kwa akili zao wenyewe
bila kuibiana majibu,inamfanya mkuu wa shule ya msingi majengo Mwl
William ngulu kusema kuwa katika mwaka huu 2014 shule yake itaongoza
tena ma kuwa ya kwanza kiwilaya katika shule za msingi za serikali.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment