Ameeleza kuwa malalamiko yao hayana
ukweli kwa kuwa kuna maneno ambayo yamezoeleka na yanaweza kutumiwa na
watu wote lakini anapoyatumia hutokea msanii aliyetumia maneno kama yale na
kudai kuwa ameiba idea yake.
Ametoa mfano wa nyimbo kama Moyo
Wangu ambao anasema baada ya kuimba wasanii wengine waliimba pia lakini
hakuwahi kujitokeza kusema ameibiwa kwa sababu neno hilo linaweza kutumika na
kila mtu kwa ufundi wake.
Diamond ameeleza pia kuhusu tuhuma
za Wababa (ingawa hakumtaja jina) kuwa alimuibia wimbo wake wa Kitorondo na
sasa anauita Mdogomdogo.
“Sitaki
niongee kwa sababu nitampa Kick…anyways nilisikia kuna mtu anasema eti hii
nyimbo yangu ya MdogoMdogo kuna mtu kaibiwa kwa neno la Kitorondo. Sasa mimi
nikuadithie story fupi…mimi nimezaliwa Tandale nimekulia Tandale, kuna bendi
ilikuwa inaitwa Tandale Modern Taarab nyimbo yao ya kwanza inaitwa Tandale
(anaimba kidogo). Ukiacha hivyo, Kitorondo ni jina ambalo ni ngoma ambayo
wanaimba hivyo (anaimba). Yaani hii ni nyimbo.
“Kuna
msanii kaichukua kaiimba kama ilivyo ile nyimbo ya mdundiko. Halafu baada ya
kusikia neno la Kitorondo kwenye nyimbo yangu akasema yeye kaibiwa nyimbo. Mimi
nimepata taarifa nikasema ana akili kweli. Yeye ndio kaenda kuiba. Mimi
nimetumia neno la Kitorondo kwa taaluma zangu za kimuziki naliingiza kwa namna
gani kama neno, yeye anasema nimemuibia yeye. Sikujisikia vizuri…halafu nikaulizwa
kila sehemu nikienda nawaambia msiniulize maswali hayo kabisa.”
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment