BALOZI wa zamani wa Vatican katika
Jamhuri ya Dominica, Monsinyori Jozef Wesolowski ametiwa hatiani na Mahakama ya
Kanisa Katoliki kwa tuhuma za kudhalilisha watoto.
Kutokana na kutiwa hatiani huko
amepokwa upadre wake. Monsinyori Wesolowski amekuwa kiongozi wa juu kuteuliwa
na Papa kutiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ya kupokwa upadri.
Taarifa ya Vatican ilisema
Monsinyori Wesolowski alikutwa na hatia na Mahakama hiyo ya Usharika wa
Mafundisho ya Imani katika siku za hivi karibuni: kwa adhabu hiyo ina maana
hataweza kutekeleza majukumu yake kama Padre.
Wesolowski amepewa miezi miwili ya
kukata rufaa. Lakini pia anakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Makosa ya
Jinai ya Vatican. Kwa kuwa ni Mwanadiplomasia wa Kipapa yeye ni raia wa mji wa
nchi hiyo.
Papa alimrejesha Vatican, Wesolowski
ambaye ni mzaliwa wa Poland Agosti 21, 2013 na kumfuta kazi baada ya Askofu wa
Santo Domingo, Kadinali Nicolas de Jesus Lopez kumueleza Papa Francis kuhusu
kuwepo kwa tetesi kuwa Wesolowski aliwadhalilisha watoto wa kiume akiwa Jamhuri
ya Dominica.
Mamlaka za Dominican hatimaye
zilianza uchunguzi lakini hazikumshtaki. Poland, pia ilianza uchunguzi dhidi ya
Wesolowski.
Wesolowski ni Ofisa wa Juu Vatican
kuchunguzwa kwa tuhuma za udhalilishaji watoto na kesi yake iliibua waswali
iwapo Vatican, kwa kumuondoka katika mamlaka ya Dominica ilikuwa ni kumlinda na
kuanzisha uchunguzi wake kabla ya mamlaka za taifa hilo la Caribbean.
Hata hivyo Vatican haijawahi kusema
iwapo Wesolowski alishawahi kujitetea kuhusiana na tuhuma hizo na hajawahi
kutoa mawasiliano yoyote kwa mawakili wake.
Kesi hiyo imekuwa ikichukuliwa kwa
umakini kwani Wesolowski alipewa upadirisho wake na Uaskofu na Papa St John
Paul 11 ambaye pia ni Raia wa Poland.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment