SHINDANO la kumpata mrembo wa mkoa
wa Geita, Miss Redds Geita 2014 limefikia tamati kwa Recho Kwila kuibuka
mshindi wa Taji hilo.
Shindano hilo lililofanyika katika
ukumbi Disire mkoani humo kwa kuwashilikisha walimbwende 11 kutoka wilaya
za mkoa wa Geita, lengo kubwa likiwa niku mpata mlibwende wa kuuwakilisha mkoa
wa Geita.
Akizungumza katika Tamasha hilo,
mgeni rasimi ambaye ni kaimu mkuu wa mkoa wa Geita Omari Manzie Magochie,
aliwataka wazazi na walezi kuwaachia watoto wao kujiunga ulimbwende kwani si
huuni kama wanavyo fikilia na kusema ni
kazi kama kazi Nyingine.
Naye mshindi huyo akizungumza baada
ya kupata taji hilo, alisema kuwa yeye atajitaidi kuwasaidia watoto wanao wa
mitaani, na kutangaza Vivutio vilivyopo katika mkoa wa Geita kikiwemo
kisiwa cha Rubondo na Madini, ili wageni wanaokuja wajue
kilichopo katika mkoa huo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment