
Akikabidhi chakula hicho, mzee
wa kanisa la Waadventista wasabato mtaa wa Kijenge Agrey
Tumaini, alisema kuwa wameamua kuwasaidia wananchi hawa kutokana na janga la
mafuriko ya maji ambapo yaliwasababishia nyumbakuezuliwa pamoja na mazao yao kusombwa na maji hayo
Alisema kuwa wao kama kikundi cha
WAMO kutoka katika kanisa hilo waliguswa sana na tatizo hili hivyo
wakaamua kujichanga na kununua vyakula ivyo na nguo kwa ajili ya wahanga hao wa
mafuriko.
Alisema kuwa wameweza kutoa gunia
kumi za mahindi ,maharage kunia tatu,unga wa ugali pamoja na nguo kwa ajili ya
watoto wa wananchi ambao walikubwa na janga hilila mafuriko.
Akipokea msaada huo, mmoja wa
wananchi hao alietambulika kwa jina la Gidion Maganga, alishukuru
kwaniaba ya jamii yao na kuongeza kuwa baadhi yao walikuwa hawajui hatima ya
maisha yao kwani ata chakula kwao kupata ni tabu .
Alisema kuwa pamoja kuwa kuna baadhi
yaviongozi na taasisi ambazo zimewapelekea chakula kama maindi ,magodoro
pamoja na nguo, bado wanaitaji msaada, kwani mvua zile ziliwachukulia vitu vyao
vingi ikiwemo mazao maindi waliokuwa wameyaifadhi ndani vyombo ,magodoro na sio
ivyo tu lakini pia zileweza kumuua mwananchi mmoja.
Alitoa wito kwa wananchi serekali
pamoja na taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuwasiaidia kwani wapo katika
halingumu sana katika kipindi hichi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment