Tukio hilo limetokea kwenye Ukumbi
wa Bunge la Kaunti ya Nairobi na kuwaacha wabunge vinywa wazi.
Katika hali isiyo ya kawaida, boksi
la kondomu lilikutwa ndani ya ukumbi huo na kuwashtua wabunge wote akiwamo
spika wa bunge hilo.
Mwakilishi wa eneo la Karura, Kamau
Thuo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuliona boksi hilo na kuwashtua wabunge wengine
hali iliyoibua mjadala mzito.
Kutokana na sintofahamu hiyo Spika
Alex Ole Magelo aliwataka wahudumu kufungua boksi hilo kujua kilichomo ndani
yake ndipo walipokuta kondomu.
“Nafahamu
wote humu ni watu wazima, lakini ninachoshangaa ni nani ambaye ameleta kondomu
hizi ndani ya ukumbi huu,” alihoji
Spika Magelo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya
Afya, Manoah Mboku aliwaondoa hofu wabunge na kueleza kuwa kondomu hizo
zilipaswa kuwekwa kwenye vyoo vya wanaume hata hivyo kwa bahati mbaya
zikapelekwa mahali kusikohusika.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment