Bw.Mussa Leonard Mdede aliyesimama |
Rais wa chuo kikuu cha CUHAS
(Bugando) na Mwenyekiti wa Shirikisho la wanafunzi vyuo vikuu nchini (TAHLISO),
Bw.Mussa Leonard Mdede ameokotwa usiku huu katika maeneo ya Usagara nje
kidogo ya jiji la Mwanza, akiwa amepoteza fahamu (hajitambui) lakini hana
majeraha yoyote na amepelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili ya
vipimo na kupatiwa matibabu.
Kwa sasa ameweza kuongea (japo kwa
taabu) lakini hakumbuki chochote kilichotokea.
Bw.Mdede alitoweka ghafla siku ya
jumatano tar.18 mwezi huu, saa kumi jioni,na haikuweza kufahamika mara moja
yupo wapi, mpaka usiku huu taarifa za kupatikana kwake zilipotolewa.
Taarifa hizi zimedhibitishwa na
Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Bw.Benjamin Thomas. Taarifa
zaidi juu ya hali ya Bw.Mdede zitazidi kutolewa kwa kadri zinavyopatikana.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa
Mwanza ameahidi kutoa taarifa leo.
SOURCE: Nicholaus Kilunga (mwandishi
aliyepo mkoani Mwanza)
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment