MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 8 June 2014

NEWS ALERT!!! CCM BUKOBA YALAANI OMBI LA FRIENDS OF BUKOBA KWA WAZIRI MKUU

Katibu mwenezi kushoto Ramadhan Kambuga, na katibu CCM manispaa Janeth Kayanda
Waandishi wa habari wawapo kazini ofisini CCM

Kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya Bukoba, imelaani na ombi la friends of Bukoba kwa waziri mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani KAGERA, katibu mwenezi CCM manispaa ya Bukoba Bwana RAMADHAN KAMBUGA, amesema kuwa kamati ya siasa ya wilaya kupityia kikao chake cha 6/6/ 2014, ilijadili kwa kina ombi la Friends of Bukoba kwa waziri mkuu, kumwomba avunje baraza la madiwani wa manispaa ya Bukoba.

Amesema kuwa pendekezo lao kwa waziri mkuu, linalengo la kufifisha maendeleo ya wananchi kwani halilengi kuleta usuruhishi ambao unatafutwa na serikali inayofuata mfumo wa Demokrasia, 

KAMATI YA ccm WILAYA Bukoba, imesema kuwa ingekuwa tayari kuwaunga mkono FRIENDS OF BUKOBA, kama wangetambua na kusimamia masuala ya ardhi, na kama wangesimamia utekelezaji ushauri uliomo kwenye taarifa ya CAG, wakiongeza kuwa hawakuwashirikisha wananchi kujua mapendekezo yao.

Hatahivyo wameongeza kuwa Frieds of Bukoba, hawajawahi kujitambulisha wala kushughulikia mgogoro wanaoutaja, hivyo chama kinashangazwa na kauli yao ya kuomba kuvunjwa kwa baraza.

Wiki iliyopita, wanaumoja wazawa wa Kagera waishio mikoani na nje ya nchi, walimwandikia waziri mkuu barua kuomba avunje baraza la madiwani, katika kipindi ambacho waziri mkuu alikwishatamka kuwa kufukuza madiwani siyo utatuzi wa mgogoro wa Bukoba.

Na Mwanaharakati.

No comments: