SERENGETI
BOYS KUCHEZA AZAM COMPLEX
Mechi ya
kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Afrika Kusini (Amajimbos)
itachezwa Ijumaa, Julai 18 mwaka huu katika Uwanja wa Azam Complex uliopo
Chamazi jijini Dar es Salaam.
Serengeti
Boys ambayo imeingia moja kwa moja katika raundi ya pili ya michuano hiyo
inatarajia kuingia kambini wiki ijayo kwenye hosteli za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, na itacheza mechi
hiyo kuanzia saa 10 kamili jioni.
Amajimbos
kama ilivyo Serengeti Boys imeingia moja katika raundi ya pili pamoja na timu
za Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Congo Brazzaville, Ethiopia, Gabon,
Ghana, Ivory Coast, Mali, Morocco, Nigeria, Rwanda, Senegal, Tunisia na Zambia.
Mechi ya
marudiano itachezwa Afrika Kusini kati ya Agosti 1na 3 mwaka huu. Iwapo
Serengeti Boys itafuzu itaingia raundi ya tatu itacheza mechi zake kati ya
Septemba 12 na 14 mwaka huu wakati marudiano itakuwa kati ya Septemba 26 na 28
mwaka huu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA
MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA (TFF)
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment