![]() |
Sheikh Mohammed Idris |
Sheikh Mohammed Idris, ambaye ni
mwenyekiti wa baraza la maimamu na wahubiri nchini Kenya, aliuawa karibu na
msikiti ulio karibu na nyumba yake na watu wasiojulikana.
Duru zinasema kwa alikuwa amepokea
vitisho kutoka kwa vijana wenye itikadi kali za kidini na tayari alikuwa
ameelezea hofu juu ya maisha yake.
Wahubiri kadhaa mashuhuri wameuawa
katika hali ya kutatanisha katika miaka ya hivi karibuni.
Wengine waliuawa kwa madai ya kuwa
na uhusiano wa karibu na kundi la wanamgambo la al-Shabaab huku wafuasi wao
wakiilaumu serikali kwa mauaji yao, madai ambayo serikali imakenusha.
Marahemu Idris alikuwa ameitaka
serikali kukabiliana na baadhi ya watu wenye itikadi kali za kidini ndani ya
msikiti hali ambayo ilisababisha baadhi ya waumini kumuita msaliti.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment