Wananchi wameendelea kuhimizwa
kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii pamoja na kuunda vikundi kwaajili
ya kupata mikopo mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa
kazi na ajira Mh. Makongoro Mahanga nakusema kuwa serikari iko katika
mchakato wa kuainisha vikokotoo kwa ajili ya ulinganisho wa gharama za michango
ya wanachama katika mifuko hiyo ili kuweka usawa katika mifuko hiyo na kuifanya
kuwa endelevu.
Pia amesema kwa sasa serikali bado
inaendelea kutoa mikopo kwa wanachama kupitia vikundi mbalimbali ambapo amesema
bado kuna mchakato wa kuangalia uwezekano wa kutoa mikopo kwa mtu mmoja mmoja.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment