MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 4 June 2014

MSANII MWINGINE BONGO MOVIE AANDIKA WOSIA




Devotha alisema akifariki asinunuliwe jeneza la kifahari, bali lichongwe kwa mbao za kawaida na lisiwekwe mapambo yoyote, watu wasilie msibani kwake na kwamba endapo vitu hivyo vitakiukwa, basi mwili wake utagoma kubebeka.

“Unajua duniani nimekuja uchi, sasa siku nikifa sitaki mbwembwe za kununuliwa jeneza la mamilioni wakati nimeacha watoto, ni bora hizo fedha wapewe wanangu ziwasaidie, vivyo hivyo pia sitaki watu walie kwa kuomboleza kwenye msiba wangu kwa sababu watakuwa wananiumiza tu, hata watoto na ndugu zangu nilishawaambia,” alisema Devotha.

Katika misiba ya hivi karibuni ya wasanii nyota, imeshuhudiwa kamati mbalimbali zikiundwa na kuchangisha fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitumika kununulia majeneza ya bei mbaya, vyakula vya gharama na shughuli zingine ikiwemo ukodishaji wa magari ya kusindikiza msafara wakati wa mazishi.
  Na Mwanaharakati.

No comments: