MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 4 June 2014

NEWS ALERT!!!WAANDISHI WA BLOG NCHINI, WAMESHAURIWA KUHARIRI HABARI ZAO KWA MAKINI KABLA YA KUZIWEKA MTANDAONI




Bwana Lawa amesema kuwa blog ni kama chombo kingine cha ahabari, hivyo taarifa zake zinatakiwa kuhaririwa kupitia misingi ya habari, akisistiza kuwa wahariri wake kwa kiasi kikubwa, wanakosea kuweka caption za picha ambazo zimekuwa zina makosa ya kisarufi na tahajia (spellings jambo ambalo linapunguza ladha ya habari na taarifa mnazo post kwenye blog.

“Kutokana na hali hiyo ninawaomba sana tena sana muimarishe uhariri wa habari hizo na hata pale mnapogundua kuwapo kwa tatizo hata kama habari tayari imekwisha pandishwa yaani up-loaded basi ishusheni  ili ifanyiwe masahihisho” alisema Lawa.

Kwa upande wao waandishi na wamiliki wa blog, wamekiri kupokea ushauri huo wa mtaalamu wa habari ambaye ahatahivyo amekuwa mshauri mkubwa wa vyombo vya habari, baada ya kushika nyadhifa mbalimbali katika vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na kuwa mkrugenzi Kasibante fm redio Bukoba.

Hatahivyo waandishi wameomba MCT kuwapa mafunzo zaidi kuhusu kuandaa habari za blog, kwani wengi hawana ujuzi wa kutosha katika hilo.
Na Mwanaharakati.

No comments: