Hali hii inashuudiwa mara kwa mara katika vituo
vidogo na vya dharura kwenye barabara kuu kote nchini.

Mwandishi wa mtandao huu, ameshuudia vitendo hivyo
katika barabara ya Dodoma- Mwanza, ambapo katika maeneo ya Ikungi Singida,
askari wa usalama barabarani walisimamisha basi la kampuni jina linahifadhiwa
na kuzungumza na watumishi wake pembeni huku wakisikika wakicheka na baada ya
hapo askari polisi aliyeonekana kuwa V tatu ambaye kijeshi anajulikana kama
SAJENTI (SAGIN ) aliingia kwenye gari akiwauliza abiria kama wamefunga mikanda
baadhi ya abiria walijibu kuwa gari halina mikanda, lakini akari huyo aliondoka
pasipokujibu chochote.
Katika mkoa wa Shinyanga karibu na chuo cha VETA,
askari wa usalama barabarani alisimamisha basi hilo, na kumuita Kondakta ashuke
na baada ya hapo walifokeana na badaye wakaanza kucheka huku askari akionekana
anaandika jambo kwenye karatasi nyeupe ambayo Konda alitaka kuchukua mara ya
kwanza askari akakataa na kurudisha mkono, mara ya pili akampa mkono kama
anataka kuchukua karatasi lakini haikuwa hivyo na badala yake wakashikana na
kuagana huku wakicheka, je aliandika ya nini kama hakiwa ya kusainiwa, na
askari kushikana mkono na mtu ambaye wamefokeana na unaoonesha siyo wa salamu
inamaana gani kwa jamii?
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment