Makachero wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wamefanikiwa kumtia mbaroni mmoja wa washukiwa wa matukio ya tindikali visiwani hapa Alawi Mohammed Silima (25) mkazi wa Fuoni Melinne nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema mtuhumiwa anahusishwa na tukio la kumwagia tindikali Sheha wa Shehia ya Tomondo mjini Zanzibar Bw. Mohammed Omar Saiidi Kidevu kabla ya kutoweka.
Inspekta Mhina amesema, Mtuhumiwa
huyo ambaye kwa muda mrefu alikuwa akisakwa na Polisi kwa kuhusina na tukio
hilo, alikamatwa juzi usiku akiwa mafichoni katika enero Fuoni baada ya taarifa
za kiintelijensia kubaini kuwepo kwake.
Bado Makachero hao wanaendelea
kumhoji mtuhumiwa huyo kwa lengo la kuubaini mtandao mzima wa matukio
mbalimbali yakiwemo ya tindikali yaliyotokea siku za nyuma visiwani humo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment