MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday 17 July 2014

NEWS ALERT!!! WAKAZI WANATIBIWA CHINI YA MTI

 
 

Wananchi wa Kijiji Cha Igenge Kata ya Saja Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Wanaendelea Kutoa Huduma ya Kliniki Kwa Watoto Kwa Kwa Kuwaning'iniza Juu ya Miti  Kutokana na Ukosefu wa Zahanati Katika Kipindi Chote Cha Miaka 50 Ya Uhuru.



Hadi Sasa Ukosefu wa Kituo Cha Kutolea Huduma ya Afya Umesababisha Kuwepo Kwa Adha Hiyo.

Wakizungumzia Tatizo hilo Baadhi ya Wazazi wa Watoto Waliokutwa Wakiendelea na Upimaji huo Kwa Kuning'iniza Mzani Katikati ya Mti Mmoja na Mwingine Wamesema Kuwa hadi Kufikia Kijiji Jirani Chenye Zahanati Kuna Umbali wa Takribani Kilomita Nne Hadi Tano.

Aidha Wamesema Kuwa Adha Hiyo Imekuwa Ikiwapa Shida Wananchi Katika Kijiji Hicho Hususani Kwenda
Katika Kijiji Cha Iramba Kilichopo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Kupata Huduma ya Afya Kwani Tangu Kijiji Hicho Kipate Usajiri Mwaka 1995 Hakijajenga Zahanati.

Viongozi wa Kijiji Hicho Akiwemo Mwenyekiti na Kaimu Mtendaji Bwana Moshi Lugoya Wamesema Kuwa Mkakati  wa Kuwanusuru   Wananchi Hao  ni Kubadili Matumizi ya Soko Lilopo Kijijini Hapo Ili Litumike Kama Zahanati na  Kwani Tangu Lijengwe na Serikali Kupitia Mradi wa TASSAF Halifanyi Kazi Yoyote Huku Wakiendelea na Mpango wa Kuandaa Tofali Kwa ajili ya Ujenzi wa Zahanati.

Kwa Upande Wake Diwani wa Kata ya Saja Bwana Saja Bwana  Andrew Mangula amekiri kutokuwepo kwa zahanati katika vijiji hivyo Vya Igenge na Idenyimembe na Kwamba Wananchi Hao Wamekuwa Wakipata Huduma Katika Kijiji Jirani Kilichopo Mkoa wa Iringa Licha ya Kwamba Huduma Hiyo Haiwahusu Kwa Mujibu wa Bajeti Vijiji vya Kata ya saja Wilayani Wanging'ombe vinakabiliwa na changamoto mbalimbali Hali Inayowapa Wasiwasi Juu ya Karne Iliyopo na Miaka 50 ya Uhuru Iliyopo Hadi Sasa.


Na Mwanaharakati.

No comments: