Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia
na maendeleo- Mh. Freeman Mbowe amesema Ukawa hauwezi kukataa mazungumzo
isipokuwa wanaweza kukataa kushiriki bunge maalum la katiba endapo masharti
waliyoyatoa hayatafanyiwa kazi ikiwemo kujadili rasimu ya pili ya katiba na si
vinginevyo.
Mh Mbowe ameyasema hayo kwenye kikao
cha kawaida cha kamati kuu ya Chadema ambacho kinatarajia kujadili ajenda 10
ikiwemo mwenendo mzima wa mchakato wa katiba ambapo amesema taifa linahitaji
katiba mpya na kwamba hawako tayari kuingia uchaguzi mkuu kwa kutumia
sheria,tume ya uchaguzi, na katiba ile ile ya zamani.
Aliyekuwa mjumbe wa tume ya
mabadiliko ya katiba Mwesiga Baregu amemtaka rais Kikwete kuvaa joho la urais
ili kunusuru mchakato huo huku akimtaka mwanasheria mkuu wa serikali kutoa
ufafanuzi juu ya sheria ya mabadiliko ya katiba wananchi na wajumbe wa bunge
maalum la katiba waielewe vizuri ili wasifanye maamuzi kinyume na sheria.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa
kikao cha kamati kuu ya Chadema waliohudhuria kikao hicho wamesema
upatikanaji wa katiba mpya haupaswi kutumia mabavu na ubabe isipokuwa ni
kwa njia ya maridhiano ya pamoja na kuongeza kuwa endapo katiba mpya
haitapatikana madhara yake ni makubwa kwa taifa hasa suala la uporaji wa
rasilimali za nchi na uwajibikaji wa viongozi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment