MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday 19 July 2014

MAAJABU TENA!!! TUNGULI KWENYE KABURI LA MSANII RACHEL HAULE

 Tukio hilo la kustaajabisha, lilidaiwa kutokea Alhamisi iliyopita katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa chanzo chetu, ndugu wa marehemu mmoja ambaye hakujulikana jina walikuwa kwenye makaburi hayo wakifanya kumbukumbu mbalimbali ndipo walipokuta ‘madongoloji’ hayo juu ya kaburi la Recho.
                                        

 
Baada ya kujionea vitu hivyo, mapaparazi wetu walikwenda kuwauliza walinzi wa makaburi hayo kama walikuwa na taarifa hizo.Mlinzi mmoja aliyeonekana kuwa ni fundi wa kuzungumza lakini bingwa wa uoga, hasa kwa kuona mauzauza ya kutisha kama hayo ndiye aliyepatikana. Akasema:


“Ah! Hivyo vitu vimetupwa na nani? Kuna watu walikuwa wakitembelea makaburi ya ndugu zao ina maana hawakuviona hivyo vitu?
“Lakini huyo mtu aliyewapigia simu mngemuuliza yeye, anaweza kuwa aliwaona walioviweka.  Mimi siwezi kwenda sasa hivi kwenye hilo kaburi.”




Ingawa mlinzi huyo alishindwa kwenda kushuhudia tukio hilo, lakini watu  waliokuwa wakisafisha makaburi ya ndugu zao walifika kwenye kaburi hilo kujionea madongoloji hayo.
Miongoni mwa waliofika na kuwa mashuhuda ni mama mmoja aliyedai ni  mlokole wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kimara- Temboni jijini Dar ambaye alikataa kutaja jina lake.
Mlokole huyo alivikemea vitu hivyo kwa Jina la Yesu kisha akasema havina tena mamlaka  ya kishetani kwa wakati huo na vimebaki kuwa takataka baada ya kuvipiga Neno la Mungu.



Shuhuda mwingine alikuwa ni kijana mmoja aliyekwenda kujengea kaburi la mteja wake ambaye alishtushwa na mauzauza hayo na kusema hali inatisha! Baada ya kijana huyo, babu mmoja aliyekutwa eneo hilo alisema vitu hivyo ni ndumba maarufu sana mkoani Tanga ambapo alisema anaifahamu ndumba hiyo ambapo wachawi walikwenda kuwangia kaburi hilo na kujaribu kuivuta nyota ya marehemu.

Babu huyo aliongeza kuwa, wachawi hao walichelewa kwani kwa kawaida kafara kama hiyo hufanywa siku saba baada ya mwili wa marehemu kuzikwa.

“Mara nyingi nyota za wafu huweza kutumiwa na watu walioko duniani ingawa wakati mwingine mtumiaji wa nyota hiyo anaweza kupatwa na madhara makubwa ikiwemo kifo cha ghafla.
“Hawa ni cha mtoto tu, walikuja kulichezea hili kaburi lakini wamechemsha,” alisema mzee huyo.


Baada ya hapo, mapaparazi wetu walimsaka aliyekuwa mchumba wa marehemu Recho, George Saguda ambaye alisema wao kama familia hawahusiki na tukio hilo na kudai hiyo itakuwa ni mipango ya washirikina. 

Na Mwanaharakati./kwa hisani ya GPL

No comments: