MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday 18 July 2014

TOBAA!!! MGANGA WA JADI AKAMATWA AKIWAVUA NGUO NA KUCHEZEA SEHEMU ZA SIRI ZA WAKE ZA WATU


 Tukio hilo la aina yake lilijiri maeneo hayo, usiku wa manane wa kuamkia Jumanne iliyopita, wakati waumini wa Dini ya Kiislamu waliofunga kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakila daku.

 
Kwa mujibu wa mashuhuda, jamaa huyo alidaiwa kuwa alikuwa akiwafanyia wake hao wa watu dawa ya mapenzi kwa kuwavua nguo zote kisha ‘kuwachezea’.
 
Ilidaiwa kuwa mbali na kuwachezea, amekuwa akiwafanyia mchezo usiofaa mmoja baada ya mwingine.

Chanzo cha sakata hilo kilidai kuwa sangoma huyo amekuwa na tabia hiyo hasa akimuona mwanamke mwenye mvuto katika hali ambayo haikueleweka mara moja humuita majina yake matatu, yaani la kwake, baba hadi la babu yake, jambo linalosababisha anayeitwa kushtuka na kuhisi mtu huyo atakuwa anamfahamu kiundani.

 


Ilidaiwa kuwa baada ya mwanamke huyo kusimama huanza kumwelezea matatizo yake na kumtajiwa hadi matatizo yanayowapata ndugu zake walio vijijini na sehemu nyingine za mbali. 

Kiliendelea kudai kwamba, sangoma huyo amekuwa akiwavuta wanawake wengi kwa kuwatajia matatizo yao sawia bila kukosea hivyo kuwachanganya na kumjengea imani kuwa ni ‘fundi’ wa masuala hayo.
 
Kufuatia vituko vyake, juzikati mume wa mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa), Huruka Hassan alirejea nyumbani kwake na kukuta mkewe hayupo.Alidai alipofanya uchunguzi wa haraka, aligundua ameenda kwenye gesti hiyo kupata tiba.

Ilidaiwa kwamba, siku zote Huruka amekuwa akimuacha mkewe akapate tiba lakini siku ya tukio machale yalimcheza, alipofika kwenye gesti hiyo alijibanza ukumbini na kusikia sauti ya mkewe ikinong'ona chumbani na sauti ya 'besi' la sangoma huyo kwa mbaaali.
 
Ilisemekana kwamba uzalendo ulimshinda Huruka na kujikuta akivunja masharti ya kilinge cha sangoma huyo kwa kuchungulia kwenye tundu la kupitisha funguo.

"Haaamadi!" alisikika Huruka alimuona laivu mkewe akiwa mtupu akitaka kufanyiwa vitendo vichafu ambapo sangoma huyo alidaiwa kuwa alikuwa akjiandaa kumfanyia ‘amshaamsha’.

Kwa upande wao, polisi walimshikilia sangoma huyo kutokana na sababu za kiusalama kufuatia wenye wake na wananchi wenye hasira kutaka kumpiga mawe na kumuua. 
 

Na Mwanaharakati.

No comments: