 |
| Meneja TANESCO KAGERA mhandisi Martine Madulu akieleza jinsi mradi huo unavyokamilishwa |
 |
| Transformer mpya yenye MVA15 |
 |
| Transformer ya zamani inayotumika sasa yenye MVA5 |
 |
| Mtaalamu kutoka makao makuu Tanesco Dar es salaam anayefunga Transformer hiyo Bwana AMON GAMBA, akitoa ufafanuzi wa kitaalamu. |
 |
| Fundi msaidizi kulia akiendelea kukunjua waya unaotumika kuweka mawasiliano ya umeme katika transformer hiyo mpya. |
 |
| Mwonekano wa Transformer mpya ya kufua umeme kwa MVA15. |
Meneja wa
shirika hilo mkoa wa kagera mhandisi MARTINE MADULU akiongea na waandishi wa
habari, amesema wananchi mkoani kagera wanatarajiwa kuondokana na
kukatikakatika kwa umeme kutokana na kufungwa transfoma mpya ya kusambaza umeme katika mkoa wa
kagera.
Bwana madulu
amesema kuwa serikali imeamua kufanya kuleta transfoma hiyo mpya iliyogharimu
zaidi ya bilioni 1.4 kutokana na kuongezeka kwa wateja na kusababisha transfoma
iliyokuwepo kushindwa kutoa huduma iliyokuwa inahitajika.
Mhandisi madulu ameongeza kuwa taransfoma hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia
wateja zaidi ya elfu 22 wa mkoa wa kagera kuliko hii ambayo ilikuwepo.
Pia
amewataka wananchi kuendelea jkushirikiana na tanesco katika kutoa taarifa kwa
wanahoujumu miundo mbinu ya shirika hilo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment