MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 19 August 2014

MUHIMU!!! JWTZ lasherehekea Miaka 50 kwa kuvisaidia vituo vya kulea watoto yatima.

Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na maafisa Jamii na wananchi wakifuatilia kwa makini risala ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleao ya Jamii ,Jinsia na Watoto Meshack Ndasikoi(hayupo katika picha), wakati wa hafla ya kufungua wiki ya kusaidia jamii ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi laWananchi wa Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Brigedia Jenerali Sarah Wambali akisoma risala ya kumkamribisha Mgeni rasmi katika hafla ya kusherekea miaka 50 ya Jeshi hilo leo jijini Dar es Salaam, ambapo wanatarajia kutoa misaada ya vyakula na vifaaa mbalimbali kwa vituo vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleao ya Jamii ,Jinsia na Watoto Meshack Ndasikoi ambaye ni mgeni rasmi katika hafla ya kusherekea miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania leo jijini Dar es Salaam na kuzindua wiki ya kusaidia jamii kwa kutoa msaada wa vyakula kwa vituo vya kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.
Na Mwanaharakati.

No comments: