MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 27 August 2014

HATARI YA VIFO VIWANDANI YAENDELEA MKOANI PWANI.

Siku chache baada ya mtanzania kugundulika amesagwa na machine na taarifa zake kutoripotiwa katika kiwanda kimoja, huku mwingine akilipukiwa na mtungi wa gesi usoni katika kinu cha kuyeyusha chuma chakavu katika kiwanda kingine, mchina mmoja naye asagwa na machine na kubaki vipandevipande.

Taarifa inasmea kuwa mchina huyo ni wa kiwanda cha SUNSHINE LTD, kilichopo mjini Kibaha Pwani, amesagwa na moja ya mashine za kiwanda hicho ambapo inasemekana mchini mwenzake aliwasha mashine hiyo bila kujua kama mwenzake yuko ndani yake kwa shughuli za kitaalamu, na wakaja gungua mashine imeshaanza kumsaga, ambapo jitiada za kumwokoa zilifanikiwa kukusanya vipande vya mwili wake tu.

Kiwanda hicho kinajishughulisha na uzalishaji wa GYPSUM, ambapo wakati jicho letu linafika pale juzi, lilikuta jitihada za kuchoma vipande vya mwili wa mchina huyo zikifanywa, huku wenzie wakijitahidi kuficha taarifa zake.

Jitiada za kuendelea kupata taarifa za viwanda na utendaji wake zinaendelea ili tukujuze yanayotendekea na kwanini, lakini je wahusika na wafanyaje katika hayo na hasa wizara ya kazi na ajira pamoja na ya viwanda na biashara.
Na Mwanaharakati.

No comments: