WATU wawili wameuawa kwa
kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana kwa imani za
kishirikina katika mkoa wa Geita.
Tukio hilo limetokea tarehe 20
mwezi huu majira ya saa mbili usiku katika kijiji cha Hililika kata
ya Bukoli wilayani Geita, Mkoani hapa.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi
Mkoani hapa Peter Kakamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja
waliouwawa kuwa ni Agines Mihayo (22) na Nyanjige Mtula(65) wote wasukuma na
wakazi wa kijijij hicho.
Kamanda Pita aliongeza kuwa Agnes ni
jirani yake na Nyanjige na siku hiyo Agnes alikwenda kwa Nyanjige kumtembelea
kama jirani yake na alipofika alikuta anakula naye alianza kula kabla
hawajamaliza inasadikika watu wasiofahamika walikuja na kuanza kuwakata mapanga
na kuwauwa palepale na kutokomea kusikojulikana.
Uchunguzi wa Tukio hilo unaendelea
ili kubaini chanzo cha tukio hilo na watuhumiwa wa tukio hilo wanatafutwa na
jeshi la polisi kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Matukio ya kuwauwa vikongwe kwa
imani za kishirikina katika Mkoa wa Geita yanazidi kushamiri huku wananchi
wakiomba serikali kuwapa kanda mahalum kama mkoa wa mara huenda matukio
ya mauaji yanaweza kupungua.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment