MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 20 August 2014

MATOKEO YA MKUTANO MKUU CCM

Umefanyika jana mjini Dodoma, ambapo watanzania walitegemea utoke na mapendekezo tofauti kuhusu bunge la katiba, lakini linaendelea kawaida bila mabadiliko.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC ,Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Katibu wa NEC Oganizesheni Dk.Mohamed Seif Khatibu akizungumza na Mjumbe wa Kati Kuu ya CCM DK. Salim Ahmed Salim ndani ya ukumbi wa mkutano wa White House kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakijadiliana kabla ya kuanza kwa kikao kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma, kutoka kushoto ni Profesa Anna Tibaijuka, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Dodoma.(Picha na Adam Mzee)
Na Mwanaharakati.

No comments: