
Uchunguzi uliofanywa na waandishi ndani ya jeshi hilo, umegundua kuwa kuna madai hayo na kwamba mchungaji huyo alitua jijini Dar na kufanya mazungumzo na Rose kwa ajili ya kwenda kutumbuiza nchini DR Congo, Julai mwaka huu katika mkutano uliohusisha wageni kutoka Ulaya na kukubaliana amlipe Dola za Marekani 5,000 (zaidi ya shilingi milioni 8).
Kwa mujibu wa chanzo, ilidaiwa kuwa
mchungaji huyo alimkabidhi Rose dola 1,900 kama utangulizi na kubaki dola 3,100
ambazo angemlipa baada ya onesho. Makabidhiano hayo yalifanyika Magomeni ya
Mwembechai jijini Dar.
Kutokana na sekeseke hilo, mwandishi
wetu alimsaka mchungaji huyo na alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa madai hayo,
alikiri na kusema alimuamini sana Rose lakini cha ajabu mambo yamekuwa tofauti
kwa kuwa hakufika kwenye tamasha.
Mchungaji huyo aliendelea kudai
kuwa, kinachomuuma zaidi ni kwamba, Rose hataki kumrudishia fedha zake na
badala yake amekuwa akimzungusha na chenga kibao.
“Siamini kabisa kama Rose angeweza
kufanya vile maana yeye ni mtumishi wa Mungu, sasa kwa nini afanye mambo yasiyompendeza
Bwana? Nashangaa sana, sijui hata ni nini kimemuharibu huyu! Nikimpigia simu
akipokea kesho haziishi.
“Anashindwa kuwa na utu maana mimi
nimeishiwa fedha naishi kwa shida hapa nchini, angenipatia hizo pesa
zingenisaidia sana maana ujio wangu huu ni kwa sababu ya kudai hizo pesa tu,
ndiyo maana nikaamua kulifikisha suala hili kwenye vyombo vya dola baada ya
kuona hatuelewani,” alisema.
Ili kuweka sawa mzani wa habari,
paparazi wetu alimtafuta Rose Muhando kupitia simu yake ya mkononi ambayo
iliita bila ya kupokelewa licha ya kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi aliamua
kukaa kimya mpaka gazeti linakwenda mtamboni.
Kesi imefunguliwa katika Kituo cha
Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa jalada namba KJN/RB/7122/14 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment