MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 23 August 2014

NEWS ALERT!!! KIKAO CHA KWANZA BAADA YA MADIWANI 6 KUSIMAMISHWA KATIKA MANISPAA YA BUKOBA

Taarifa zilizopo, zinasema kuwa baraza la madiwani litakaa jumatatu 24August 2014, katika kikao walichoita cha dharura, na taarifa kuhusu kitakachozungumzwa hazijawekwa bayana.

Ikumbukwe kuwa mahakama ya wilaya Bukoba kuwavua udiwani madiwani wa kata 6 za Ijuganyondo, Kitendaguro, Kashai, Nyanga, na wa viti maalumu katika manispaa ya Bukoba, na kufanya idadi ya wajumbe kupungua, siku chache baada ya CAG kutoa taarifa yake ya uchunguzi, iliyosababisha wizara ya TAMISEMI kumtaka aliyekuwa Meya wa manispaa hiyo kujipima na kuachia madaraka.

Kikao cha jumatatu, kinatarajiwa kufanyika chini ya makamu Meya mzee Alexander Ngalinda na kuudhuriwa na madiwani 18 badala ya 24 wakiwamo wabunge wa kuchaguliwa na wa viti maalumu.
Na Mwanaharakati.

No comments: