Mzunguko wa nane wa tamasha la
michezo ya Majeshi na Utamaduni kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
imefunguliwa rasmi tarehe 20 Augusti 2014 na Makamu wa Pili wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Ally Seif Iddi katika
Uwanja wa Amaan mjini Unguja.Kaulimbiu ya michezo hii ni Jamii Moja, Hatma moja
kupitia Michezo ya Majeshi na Utamaduni 2014,ambapo nchi shiriki ni wenyeji
Tanzania,Burundi,Kenya,Rwanda na Uganda.
Sherehe hizo za ufunguzi pia
zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
pamoja na Mkuu wa Majeshi wa Tanzania Jenerali Davis Aldolf Mwamunyange
pamoja na wawakilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katika ufunguzi huo mgeni rasmi
alisema lengo la michezo hii ni kuyaweka pamoja majeshi ya nchi za jumuia ya
Afrika mashariki ikiwa na dhana ya kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa
majeshi haya.Mgeni rasmi aliwataka pia wanamichezo wote kuzingatia nidhamu
ndani na nje ya viwanja vya michezo.
Aliongeza
kuwa kupitia michezo hii tutaweza kuijenga jumuiya tunayoitaka kwa uthamani
wake na umuhimu wake,tunataka kuendelea kuijenga jumuia itakayokuwa ikijali
ustawi wa jamii iliyo ndani na nje ya jumuiya ili hatimaye nchi zetu ziwe
sehemu salama kwa ustawi wa vizazi vya sasa na vijavyo.
Baada ya nasaha hizo ulifuata mchezo
wa mpira wa miguu kati ya Tanzania na Burundi ambapo Tanzania lishinda magoli 3
-1 magoli ya JWTZ yakifungwa na Aidani Michael katika dakika ya 13,goli la pili
likifungwa na Abdalah Mussa katika dakika ya 25 na Amosi Mgisa akifunga goli la
tatu katika dakika za nyongeza.Na goli la Burundi likifungwa na Francis katika
dakika ya 45 kipindi cha kwanza.
Siku ya Alhamisi tarehe 21 August
2014 kulifanyika michezo saba, ambapo Tanzania ilicheza michezo miwili,
mchezo wa pete Tanzania ilicheza na Burundi katika uwanja wa Jeshi la Kujenga
Uchumi (JKU) na kushinda magoli 113- 10 na katika uwanja wa Gymkhana kulikuwa
na mchezo wa mpira wa Kikapu Tanzania na Rwanda na JWTZ kushinda
mchezo huo kwa magoli 67 – 56.
Siku ya Ijumaa tarehe 22
Agosti 2014 kulifanyika michezo saba, katika uwanja wa Amaan JWTZ
(Tanzania) ilicheza na Rwanda na kupata ushindi wa magoli 2-0, na katika mpira
wa pete Tanzania ilimenyana na Rwanda na kushinda kwa kishindo kwa magoli 95-
12, aidha katika uwanja wa Gymkhana Tanzania ilicheza na Burundi katika mpira
wa kikapu na kushinda magoli 54-51 na katika uwanja wa Migombani Tanzania
ilicheza na Kenya na kupoteza mchezo huo kwa kufungwa magoli 26- 20.
Siku ya Jumamosi Augusti 24
kulifanyika mbio za nyika kwa wanaume kilometa 12 na wanawake kilometa 8.
Praiveti Ismail Juma wa JWTZ (Tanzania) aliweza kuibuka mshindi wa kwanza
baada ya kukimbia kwa muda wa dakika 36;49;33 akifutiwa na koplo Kipimo
Kimutai wa Kenya aliyetumia mda wa dakika 37;12;06 huku mshindi wa tatu akiwa
Muhitila Felisiani wa Rwanda akitumia dakika 37;20;17.
Katika mbio za nyika kilometa 8
wanawake Kenya ilifanikiwa kushika nafasi zote tatu za juu huku praiveti
Jackline Sakilu wa Tanzania akishika nafasi ya nne, na katika uwanja wa
migombani ulifanyika mpira wa mikono kati ya Tanzania na Burundi na
Tanzania kushinda kwa magoli 25 -20. Michezo hiyo itaendelea siku ya Jumatatu
tarehe 25 Agosti 2014 katika viwanja mbalimbali.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment