Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo imesema watu wawili wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola, uliolipuka
kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.
Hao ni wagonjwa wa kwanza wa Ebola
kuripotiwa nje ya Afrika Magharibi tangu kuzuka kwa ugonjwa huo huko, ingawaje
haijaeleweka wazi kama vifo vya watu hao vinahusiana na mlipuko wa Ebola katika
nchi za Afrika Magharibi.
Mpaka sasa watu 1,427 wamekufa
kutokana na maambukizo ya virusi vya Ebola.
Shirika la Afya Duniani, WHO
limesema kasi na kiwango cha milipuko hiyo hakijawahi kutokea hapo kabla.
Watu wanaokadiriwa kufikia 2,615
Afrika Magharibi wameambukizwa ugonjwa wa Ebola tangu uzuke mwezi Machi mwaka
huu.
Hakuna tiba inayojulikana kutibu
ugonjwa huu lakini baadhi ya watu walioambukizwa virusi vya Ebola wamepata
nafuu baada ya kupewa dawa ya Zmapp iliyo katika majaribio.
Hata hivyo dawa hiyo imeadimika kwa sasa.
Hata hivyo dawa hiyo imeadimika kwa sasa.
Pia Jumapili, mfanyakazi wa afya wa
Uingereza aliambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone na kurejeshwa
Uingereza akisafirishwa na ndege ya jeshi la Uingereza, RAF.
Ni mgonjwa wa kwanza Mwingereza kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola wakati wa mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo.
Ni mgonjwa wa kwanza Mwingereza kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola wakati wa mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo.
Marekani imetuma vifaa vya tiba
kusaidia kupambana na mlipuko wa Ebola nchini Liberia.
Watu kadha wamekufa katika kipindi
cha mwezi uliopita baada ya kuugua homa isiyojulikana katika jimbo la Equateur
katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Jumapili, Waziri wa Afya wa DR Congo
Felix Kabange Numbi amesema watu wawili kati ya wanane waliopimwa ugonjwa Ebola
wamethibitika kuambukizwa ugonjwa huo.
Ameiambia BBC kuwa eneo la karantini
litawekwa katika eneo la kipenyo cha kilomita za mraba 100 katika eneo la
Boende ambao wagonjwa wamegundulika.
Amesema huu ni mlipuko wa saba wa
ugonjwa wa Ebola nchini DR Congo.
Virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa mara
ya kwanza viligundulika nchini humo mwaka 1976 karibu na Mto Ebola.
Bwana Numbi amesema vipimo zaidi
vinafanyika.
Nchi hiyo tayari imepiga marufuku
safari za ndege kwenda na kutoka Sierra Leone, Liberia na Guinea.
Gabon, Senegal, Cameroon na Afrika
Kusini zimechukua hatua kama hizo.
Shirika la Afya Duniani linasema
upigaji marufuku safari za ndege hakusaidii, na kinachotakiwa ni madaktari
zaidi na maafisa kusaidia kuwafuatilia walioambukizwa Ebola, ikiwa ni pamoja na
kuwa na maabara zaidi za kuhama.
Wiki iliyopita, madaktari wawili wa
Marekani waliruhusiwa kutoka hospitalini nchini Liberia baada ya kupewa dawa ya
ZMapp drug, wakati ambapo madaktari watatu wa Liberia pia wanaendelea vema.
Ugonjwa wa Ebola unaenezwa kati ya
binadamu kwa kugusana moja kwa moja na majimaji ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa
huo. Ni moja kati ya magonjwa hatari kuliko yote duniani, ambapo asilimia 90 ya
watu wanaoambukizwa ugonjwa wa Ebola hufariki dunia.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment