Kikao
hicho, kilichokutana chini ya Naibu Meya Alexander Ngalinda, madiwani hao mazungumzia
hoja ya kutenga kata ili kufikisha huduma karibu na wananchi na kupendekeza
majina yatakayotumika baada ya kutengwa kwa kata hizo.
Kata
zinazopendekezwa kutengwa, ni kata ya Bakoba na kata ya Kashai, ambapo manispaa
imetoa nafasi kwa watendaji wa kata kufanya tathmini ya kuweka mipaka katika
maeneo yanayokusudiwa kutengwa.
 |
Naibu meya Mh. Alexander Ngalinda, mkuu wa wilaya Bi Zporah Pangani katikati na mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mh Balozi Khamis Kagasheki. |
 |
Kaimu mkurugenzi Robert Kwela akitaja Agenda za kikao hicho. |
 |
Mkuu
wa wilaya ya Bukoba Bi. Ziporah Pangani,
amewashukru wananchi wa manispaa hiyo, kwa kuwa wavumilivu wakati ambao vikao
vilikuwa havifanyiki.
|
Bi.
Pangani amewataka wananchi kuwa wamoja wakati wa kuanza kutekeleza masuala
yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho leo.
 |
Nafasi aliyopangwa aliyekuwa meya wa manispaa ya Bukoba wakati huo Mh. John Aman |
 |
Baadhi ya madiwani na watalaamu wa manispaa ya Bukoba wakifuatilia kikao. |
 |
Baadhi ya viongozi watendaji wa manispaa ya Bukoba wakifuatilia kikao kilichoongozwa na naibu Meya Alexander Ngalinda. |
 |
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Bw. Shilejei, akisalimiana na katibu wa CCM manispaa ya Bukoba Bi Janet Kayanda aliyekumbatiwa amevaa nguo nyeus na kitambaa. |
 |
Waandishi wa habari wakiwa nje ya ukumbi wa manispaa ya Bukoba, baada ya kutoka nje wakati wajumbe wa kikao wakijadili hali ya awali ya mgogoro wa manispaa hiyo wakati huo. |
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment